Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imesema mvua za masika zitaendelea kuwepo hadi mwezi wa tano huku wakazi wa mabondeni wakiendelea kutahadharishwa.
Kauli hiyo imezungumzwa na meneja wa uendeshaji wa vituo vya hali ya hewa, Bi. Hellen Msemwa, ambapo amesema maeneo machache sana yanatarajiwa kupata vipindi vifupi vya mvua kubwa.