Back to top

MFANYABIASHARA CHIPUKIZI PEDIMA AENDELEA KUNG’ARA KATIKA UBUNIFU NA UO

28 November 2025
Share

#HABARI: Mfanyabiashara chipukizi, Peter Didas Mallya maarufu kama PEDIMA, ameendelea kuibua mvuto mkubwa katika tasnia ya biashara nchini kutokana na ukuaji wa kasi wa kampuni zake pamoja na mchango wake katika sekta za kifedha, teknolojia, afya na ajira kwa vijana.

Kupitia kampuni zake Pedima Enterprises, Pedima Microfinance, Pacify Limited na LocalPesa Limited, PEDIMA amejiimarisha kama mmoja wa vijana wanaoongoza mageuzi ya kidijitali na kutoa huduma bunifu zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Akizungumzia safari yake ya ujasiriamali na maono yake kwa taifa, PEDIMA alisema anaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini.

“Ninaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa. Lengo langu ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira, na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini,” alisema.

Ameeleza kuwa kampuni zake zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika jamii kupitia ubunifu unaolenga kutoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali za wananchi. 

“Pedima Enterprises inatoa huduma za super-agency na mobile money aggregation ikiwawezesha mawakala na wafanyabiashara kufanya miamala kwa urahisi zaidi,” alisema.

Akifafanua kuhusu Pedima Microfinance, PEDIMA alisema taasisi hiyo imekuwa nguzo muhimu kwa vijana na wafanyabiashara wadogo kupitia mikopo nafuu na elimu ya ujasiriamali.

Kwa upande wa LocalPesa Limited, amesema kampuni hiyo imejikita katika kubuni mifumo ya malipo ya kidijitali na huduma za kifedha mtandaoni, hatua inayoongeza ushirikishwaji wa kifedha nchini. 

Kuhusu Pacify Limited, amesema kampuni hiyo inatengeneza bidhaa za afya ikiwemo Pacify Organic Pads, zinazotoa suluhisho salama, bora na nafuu kwa wanawake.

Katika kipindi cha miaka michache, mafanikio ya PEDIMA yamempa tuzo mbalimbali za ndani na kimataifa, zikiwemo 2023 FOYA Founder of the Year Under 30; 2024 Africa Company of the Year Awards (Company to Watch of the Year); 2024 CEO Top 100 Awards (CEO of the Year); 2025 Africa Company of the Year Awards (Fintech Company of the Year); 2025 Global Recognition Award Winner; na 2025 CEO Top 100 Awards (CEO of the Year – mara ya pili).

Peter Didas Mallya alizaliwa tarehe 15 Desemba 1992 jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa Business Administration na mwanzilishi wa makampuni manne yanayokua kwa kasi nchini. Anasifika kwa uongozi, maadili ya kazi na ubunifu unaolenga kutatua changamoto za kijamii.