Back to top

Kampuni ya Solkit inayosambaza vifaa vya umeme jua yapigwa marufuku.

21 April 2018
Share

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi ATASHASTA NDITIYE amepiga marufuku kampuni ya Solkit inayosambaza na kuuza vifaa vya umeme -jua kwa wananchi wa Jimbo la Muhambwe, Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Mheshimiwa NDITIYE amesema hayo akiwa kwenye ziara jimboni kwake Muhambwe wakati akiwahutubia wananchi alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Busunzu, Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Aliwasili Wiayani humo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa kwenye Wilaya hiyo ambapo alijumuika na wananchi kukimbiza Mwenge na kukagua na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo wilayani humo.

Amesema Kampuni ya Solkit ni kampuni binafsi inayouza na kusambaza vifaa vya umeme- jua kwa wananchi wa jimbo lake hilo kwa gharama kubwa ambazo ziko nje ya uwezo wa wananchi kwa kuingia nao mikataba ya utata isiyokuwa na uwazi.

Mikataba hiyo inawataka wananchi walipie Shilingi Elfu-38 kwa ajili ya kununua vifaa vya kampuni hiyo na kuendelea kulipia Shilingi mia saba kwa siku kwa kipindi cha mwaka mzima kwa muda wa miaka mitatu.