Back to top

"TAFITI ZILENGE KUONGEZA THAMANI MAZAO YA MIFUGO"DKT.BASHIRU

15 December 2025
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kuhakikisha tafiti zake zinalenga kuongeza thamani ya mazao ya Mifugo ili kukidhi masoko ya nje ya Nchi.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo aliyoifanya, jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ulioelekeza ufugaji wa kisasa, kibishara na wenye tija.

Kadhalika Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameitaka taasisi hiyo kufanya tafiti zinazohusu uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo amesisitiza ushirikiano wa kitafiti wa Taasisi za Wizara yake na ile ya Maji ili kuboresha eneo la malisho ya Mifugo na Maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Erick Komba amesema kuwa maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Balozi Dkt. Bashiru yapo kwenye miongozo mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za kitafiti hivyo ameahidi yeye pamoja na timu yake kufanyia kazi maelekezo hayo.