Back to top

WADAU DUNIANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE MADINI

11 February 2026
Share

Sekta ya Madini Tanzania kupitia Kongamano la Mining Indaba 2026 imeendelea kuimarisha nafasi yake Kimataifa, huku Tanzania ikiendelea kujidhihirisha kama kimbilio la uwekezaji katika Sekta ya Madini kwa kuvutia mashirika ya Kimataifa, kampuni mbalimbali na wawakilishi wa kidiplomasia. 

Februari 10, 2026, Waziri wa Madini alikutana na wadau muhimu ikiwemo Benki ya Dunia katika vikao vya pembeni vya kongamano linaloendelea jijini Cape Town, Afrika Kusini, pamoja na kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Madini wa SADC.
 
Katika kikao kilichofanyika baina ya ujumbe wa Australia na Tanzania, Naibu Balozi wa Australia Christopher Ellinger alieleza kuvutiwa na mwenendo wa Sekta ya Madini nchini na kusema kwamba kwa kampuni za Australia, Tanzania ni moja ya machaguo ya kwanza kwa uwekezaji. 


Benki ya Dunia imetambua sekta ya madini Tanzania kama eneo la kimkakati lisilopaswa kuachwa pembeni katika juhudi za maendeleo na uwekezaji, ikiashiria uhitaji wa kuendelea kuwekeza na kushirikiana na serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuongeza faida za kiuchumi.


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisisitiza kwamba kaulimbiu ya “Madini ni Maisha na Utajiri” inaweka kipaumbele cha kufanya tafiti za jiosayansi na kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi. 


Aliyasema hayo alipokutana na Kampuni ya Faru Graphite inayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Black Rock Mining inayotarajia kuchimba madini ya kinywe, katika eneo la Mahenge, Wilayani Ulanga, Mkoani Morogoro. 

Katika kikao na Waziri Mavunde, kampuni ya uchimbaji madini na ukodishaji wa vifaa vya uchimbaji ya Plantcor Mining yenye makazi yake nchini Afrika Kusini ambayo ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kusaini Mkataba na Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) ilimhakikishia Mhe. 

Kampuni ya Breakthrough Attorneys na benki ya NMB, zimeshirikiana kuandaa na kutekeleza warsha ya kuitangaza sekta ya madini na kuvutia uwekezaji nchini Tanzania. 
Warsha hiyo iliyofanyika Februari 10, 2026 jijini Cape Town nchini Afrika Kusini na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kutoka sehemu mbalimbali duniani.