Back to top

MARUFUKU KUTUMIA FEDHA KAMA PAMBO VALENTINE-BOT

13 February 2026
Share

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa onyo kali kwa wananchi wanaotumia fedha kama mapambo au zawadi za Valentine, ikisema ni kinyume cha sheria na kunasababisha uharibifu wa noti.

Akizungumza Dodoma, Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema matumizi hayo yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha sikukuu, hali inayosababisha hasara kubwa kwa Taifa.

Amesema noti zinazofungwa kwenye mashada ya maua hupoteza ubora wake kutokana na gundi na mikunjo, na hivyo kushindwa kutumika kwa muda mrefu.

“Fedha ni alama ya Taifa. Kila Mtanzania ana wajibu wa kuzilinda,” amesema.

BoT imewataka wananchi kutumia njia mbadala za kutoa zawadi, ikiwemo bidhaa au fedha zilizo katika hali yake halisi.