Back to top

MFUMO WA IDRAS KUONGEZA UWAZI KODI

25 February 2026
Share

Meneja wa Ukaguzi wa Sekta za Umma, kutokea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bi. Rosemary Ruganuza
amezitaka taasisi za sekta ya umma kutumia kwa usahihi Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati akifungua  mafunzo ya mfumo wa IDRAS yaliyoandaliwa na Idara ya Walipakodi Wakubwa wa TRA kwa taasisi za umma.

Bi. Ruganuza amesema matumizi sahihi ya mfumo huo yatasaidia taasisi za umma kutekeleza majukumu yao ya kikodi kwa wakati, kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria na kanuni za kodi.

Amesema IDRAS ni sehemu ya mageuzi ya kidijitali yanayolenga kurahisisha huduma za kikodi, kupunguza makosa ya kibinadamu na kuongeza ufuatiliaji wa taarifa za walipakodi kwa njia ya kielektroniki.

“Matumizi sahihi ya IDRAS yataimarisha uwajibikaji, kuongeza uwazi na kuhakikisha majukumu ya kikodi yanatekelezwa kwa wakati na kwa usahihi. Ni wajibu kwa kila taasisi kuwa balozi wa ndani ya eneo lake la kazi,” asema Bi. Ruganuza.