Back to top

Benki ya dunia yaridhishwa na TASAF nchini.

21 April 2018
Share

Wafadhili pamoja na Benki ya Dunia wameridhishwa na utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaosimamiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF) baada ya kukagua maeneo mbali mbali nchini kisha kupata taarifa za wanufaika wa mpango huo kabla ya kuanza kwa awamu nyingine.

Akizungumza katika kijiji cha madumu kilichopo kata ya chekelei wilayani Korogwe baada ya wafadhili kutoka Mashirika ya Kimataifa kutembelea na kujionea shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa mpango huo, Mkurugenzi mtendaji wa tasaf nchini Ladslaus Mwamanga amesema hadi sasa wamefikia utekelezaji kwa asilimia 70% ya vijiji vilivyopo nchini bado vijiji zaidi ya 5300 kuingizwa katika mpango huo awamu ya tatu.

Katika utekelezaji wa mpango huo mtaalam wa masuala ya kijamii kutoka benki ya dunia Muderis Mohamed amesema wameridhishwa na mpango huo hivyo wataendelea kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kuipatia mikopo ya gharama nafuu ili azma ya kupunguza umasikini iweze kufikiwa.

Baadhi ya makundi ya akina mama walionufaik na mpango huo ameishukuru serikali pamoja na Mashirika wahisani kwa kupunguzia changamoto za maisha baada ya kuingia katika mpango huo.