
Timu ya Wataalam kutoka Idara ya Wanyamapori na Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii wameendelea na zoezi la kutoa elimu kuhusu Wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na uhifadhi wa mazingira kwa Wanafunzi wa shule za msingi na Sekindari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu katika shule za msingi Mzeri na shule ya sekindari Misima Kiongozi wa Wataalam hao Bw. Nassor Wawa amesema elimu inapotolewa kwa vijana wenye umri mdogo inasaidia kujenga utamaduni wa Uhifadhi sambamba na elimu hiyo kudumu kwa jamii kwa muda mrefu.
Ameongeza kuwa Wanafunzi hao wanapokuwa na uelewa wa kutosha husaidia kuwaelimisha wazazi na jamii kwa ujumla.

Nao baadhi ya Wanafunzi na walimu waliopata mafunzo hayo wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutoa elimu hiyo kwani imewaongezea maarifa ya namna ya kuishi na kukabiliana na Wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Wameomba elimu hiyo kutolewa mara kwa mara kwa jamii zinazunguka Hifadhi za Taifa kwa kiwa itasaidia kujenga uwajibikaji wa pamoja.
Elimu hiyo inatolewa kwa wananchi wa Wilaya ya Handeni hususani Wanafunzi wa shule za msingi na sekindari kwa lengo la kuwapa mbinu na maarifa ya kukabiliana na Wanyamapori wakali na waharibifu wanapopita katika makazi yao lakini pia kusaidia uhifadhi.
