Back to top

MAPATO AIRTEL YAFIKIA BILIONI 6.4 DATA YACHOCHEA FAIDA

09 May 2026
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Africa, Sunil Taldar, amesema Matumizi ya Intaneti na huduma za fedha kupitia simu yamekuwa injini kuu ya ukuaji wa Airtel Africa, huku kampuni hiyo ikitangaza ongezeko kubwa la mapato na faida kwa mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2026 na faida halisi imepanda zaidi ya mara mbili hadi dola milioni 813, kutoka dola milioni 328 mwaka uliopita, ongezeko hilo limetokana na ukuaji wa mapato ya uendeshaji na faida za ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Amesema Mapato ya kampuni yamepanda kwa asilimia 29.5 kufikia *dola bilioni 6.42  Kwa sarafu thabiti, ukuaji huo ni asilimia 24, na kwamba matokeo hayo yanaonyesha msingi imara wa biashara na utekelezaji wenye nidhamu na matumizi ya huduma za kidijitali na uwekezaji wa mtandao ndiyo nguzo kuu za ukuaji.

Kadhalika amesema Idadi ya wateja wa Airtel Africa imeongezeka kwa asilimia 10.5 hadi milioni 183.5 ongezeko kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa na kampuni.

Amebainisha kwamba Wateja wa huduma za data wamefikia milioni 84.2 , huku matumizi ya simu janja yakipanda hadi asilimia 49.5, matokeo yake, matumizi ya data kwa kila mteja yamepanda hadi *GB 8.9 kwa mwezi* kutoka GB 7.0 mwaka uliopita na mapato ya data yamepanda kwa asilimia 35.2 kwa sarafu thabiti na sasa ni chanzo kikuu cha mapato.

Huduma za Airtel Money zimekua kwa kasi Wateja wameongezeka kwa asilimia 21.3 kufikia milioni 54.1, huku thamani ya miamala kwa mwaka ikipanda asilimia 49 na kufikia zaidi ya dola bilioni 215 katika robo ya nne pekee. Mapato ya Airtel Money yamepanda kwa asilimia 28.4 kwa sarafu thabiti, yakiendeshwa na malipo ya kidijitali, huduma za wafanyabiashara na miamala ya kimataifa.

Aidha Sunil ameeleza faida kabla ya riba, kodi na makato (EBITDA) imepanda kwa asilimia 30.4 hadi dola bilioni 3.16 huku kiwango cha faida kikifikia asilimia 49.3, faida ya uendeshaji imepanda asilimia 45.1 hadi dola bilioni 2.12, na faida kwa kila hisa (EPS) imepanda hadi senti 18.6 kutoka senti 6.0.

Uwekezaji wa mtaji umeongezeka asilimia 31.9 hadi dola milioni 884 ukilenga upanuzi wa mtandao, kampuni imejenga vituo vipya 3,250 na kuongeza kilomita 3,200 za nyaya za fiber, mtandao wa 4G sasa unapatikana katika asilimia 98.5 ya vituo vyote, na vituo 3,100 vya 5G vinafanya kazi katika masoko sita hivyo Airtel inatarajia uwekezaji hadi dola bilioni 1.1 mwaka wa fedha 2027 ili kuimarisha miundombinu ya kidijitali na mtandao wa kasi, hivyo Airtel Africa imesema mahitaji ya huduma za kidijitali bado yako juu katika masoko yake 14, licha ya changamoto za mfumuko wa bei na mabadiliko ya sarafu, hususani Nigeria.