
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amerejesha furaha kwa Bi. Federica Masangasi wa Kijiji cha Muungano wilayani Mpwapwa kwa kumpatia godoro na kitanda.
Bi. Federica alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara na kuandika kero yake ya kutekelezwa na mumewe, Bw. Erenei Ngilikule tangu mwaka 2011 na kumuachia watoto sita.
Akielezea kero hiyo, Bi. Federica alisema mumewe ambaye ni mwalimu, alimtelekeza bila matunzo ya watoto na hata alipofikishwa kwa mtendaji hakutekeleza maagizo aliyopewa. Aliomba apewe kitanda na godoro kwa sababu yeye na wanaye wanalala kwenye salfeti.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika stendi ya Kibakwe, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma. Akiwa hapo alisikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
