Back to top

Mkurugenzi Bodi ya Korosho asimamishwa kazi

22 April 2018
Share


Waziri wa Kilimo nchini Dkt. Charles Tizeba amesitisha mkataba wa mkurughenzi mkuu wa bodi ya Korosho nchini kwa kile alichokisema haridhishwi na mwenendo na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu huyo na kusema muda wowote atatangazwa atakayekaimu nafasi hiyo.

Dkt. Charles Tizeba  ametangaza maamuzi jana usiku katika mkutano wake na waandishi wa habari katika ofisi za wizara ya kilimo mjini dodoma.