Back to top

WAZIRI KIJAJI ATEUA WAJUMBE WA BODI YA TAFORI

22 July 2026
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania, TAFORI, kufuatia uteuzi wa Profesa Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya TAFORI Sura ya 277.

Walioteuliwa kuwa wajumbe ni Daniel Charles Pancras, Profesa Dos Santos Aristariki Silayo, Dkt. Amos Mahunda Nungu, Bi. Felister Steven Lelo, Profesa Donatha Damian Tibuhwa, Jasper Lazaro Makala na CPA Beatrice Musa Lupi.


Aidha, Dkt. Revocatus Petro Mushumbusi ameteuliwa kuwa Katibu wa Bodi hiyo.

Uteuzi wa wajumbe hao ulianza rasmi Julai 17, 2026.