
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana. Abasi Kandoro Amefariki jana katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Awali Marehemu Kandoro alikuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, kabla ya kustaafu utumishi wa Umma.
Marehemu Kandoro aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Mkoa katika mikoa sita ya Tanzania bara ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Mahala pema.