Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika msikiti wa Manyema Kariakoo kushiriki swala maalumu ya kumuaga aliyewa wahi kuwa mkuu wa mkoa wa mikoa kaadha hapa nchini Bwana Abbas Kandoro aliyefari katika hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya jana wakati akiendelea kupokea matibabu baada ya kusumbuliwa kwa muda mfupi na maradhi ya vidonda vya tumbo pamoja na Kongosho.
Mbali na wananchi kujitokeza viongozi mbalimbali wa dini na wanasiasa pia walihudhuria swala hiyo iliyongozwa na Sheikhe Hamidu Jongo wa msikiti wa Manyema huku Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakary Zuber akisema taifa limepoteza kiongozi aliyekuwa mfano wa kuigwa kwa kujali na kusikIliza shida za wananchi wa chini na kuzifanyia kazi wakati akiwa mtumishi wa serikali kwa nafasi ya ukuu wa mkoa.
Wakiongea na ITV kwa nyakati tofauti baada ya mwili wa Marehemu Kandoro kuwasili katika Msikiti wa Manyema majira ya saa saba mchana baadhi viongozi waliowahi kufanya naye kazi akiwemo meya wa zamani wa Dar es Salaam Mh.Adamu Kimbisa amesema taifa limepoteza kiongozi aliyependa maendeleo ya kukua kwa uchumi wa wananchi.
Naye msemaji wa familia na mtoto wa kiume wa Marehemu Kandoro Bwana. Hussein Kandoro amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na vidondo vya tumbo na Kongosho.
Marehemu Abbas Kandoro aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya alizaliwa katika kiji cha ihemi kata ya Mgama wilaya ya Iringa vijiji Tarehe 9 mwezi 9 mwaka 1950 ameacha watoto watano na mke mmoja na anatajiwa kuzikwa kesho saa kumi katika shamba lake la Ihemi mkoani Iringa.