Back to top

Waliovunjiwa na kuwekewa alama -X kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria.

30 April 2018
Share

Serikali imesema italipa fidia kwa mujibu wa sheria kwa wananchi wote waliovunjiwa na kuwekewa alama -X- kwenye nyumba zao ambao wamekumbwa na mabadiliko ya sheria mpya barabara ya mwaka 2007.

Akijibu swali la Mbunge wa kilwa Kusini mhe Selemani Bungara  amesema serikali ina mpango gani wa kulipa fidia na kuwatafutia maeneo mengine wananchi waliowekewa alama X.

Naibu Waziri wa Ujenzi mhe.Eliasi kuandikwa amesema serikali kupitia wakala wa barabara TANROAD imefanya zoezi la kuainisha maeneo yaliyoathirika na sheria mpya ya barabara yaliyondani ya mita 22.5 hadi mita 30 kutoka katika kila upande  wa barabara.

Amesem sheria ya barabara ya mwaka 1932 ilifanyiwa marekebisho mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007 ambapo eneo la hifadhi ya barabara lilibadirika kutoka mita 22.5 kutoka katikati ya barabara kila upande wa barabara kuu hadi na za mikoa kuwa mita 30,hivyo kufanya eneo la hifadhi ya barabara kuwa mita 60 badala ya mita 45.