Back to top

Wafanyabiashara wasioridhika na maamuzi ya TRA kwenda Wizara ya Fedha

03 May 2018
Share

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara wote nchini wasioridhika na maamuzi ya kitengo cha kusikiliza malalamiko cha Mamlaka ya Mapato nchni TRA kwenda Wizara ya Fedha ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.

Akijibu swali la Mbunge wa Tunduma Mhe.George Mwakajoka katika kipindi cha papo kwa papo kwa Waziri Mkuu aliyeuliza serikali inatoa kauli gani kwa wafanyabiashara wanaongezewa kodi kubwa na wanaofungiwa biashara zao wakati sera ya serikali ni kuhamasisha uwekezaji.

kuhusu swali la Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbless Lema aliyehoji kauli ya serikali kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ya kula kwa asilimia 15 huku meli mbili zilizokuwa na shehena na mafuta zimezuiliwa bandarini na Mamlaka ya Mapato hali inayosababisha mfumuko wa bei. 

Aidha kuhusu changamoto ya kupanda kwa bei ya sukari kama ilivyoulizwa na Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Abdallah Bulembo mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imetoa vibali vya kuingizwa sukari nchni ili kupunguza kupanda kwa bei na itahakikisha inasambazwa hadi katika ngazi ya vijiji.

Kwa upande wake,Mbunge wa Ilala Mheshimiwa Mussa Zungu amehoji serikali ni lini Shirika la nyumba litakaa na chama cha wapangaji wa shirika la nyumba ili kututaua changamoto ya ongezeko la kodi pamoja na vitendo vya kuwaondoa wazee walikaa katika nyumba hizo kwa muda mrefu.