
Rais wa Zimbabwe Bwana. EMMERSON MNANGAGWA yupo katika hatari ya kutoungwa mkono na waliokuwa wapigania uhuru wa nchi hiyo na hivyo kushindwa kwenye uchaguzi unotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Mpigania Uhuru ambaye pia ni Mshauri maalum wa Rais, Bwana CHRISTOPHER MUTSVANGWA ameonesha wasi wasi huo alipokuwa akizungumza na maafisa kadhaa wakiwemo mawaziri waliokosa nafasi ya kugombea kwenye majimbo ya ubunge kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai mwaka huu.
Bwana MUTSVANGWA aliyetarajiwa kukiwakilisha chama cha ZANU-PF katika Mji wa Norton, Magharibi mwa Harare ameshindwa na kijana mpya, Bwana LANGTON MUTENDEREKI.
Naye Msemaji wa Wapigania Uhuru, Bwana DOUGLAS MAHIYA ameripotiwa kuwa katika hali ngumu kutetea kiti chake cha Harare Kusini.