Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Ruvuma umesaidia mifuko 200 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wanaopoteza maisha wakati wakifuata huduma ya upasuaji wilayani Songea.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) mkoa wa Ruvuma Bw.Abdiel Mkaro amesema kuwa wameamu kusaidia mifuko hiyo ya saruji baada ya kuona wajawazito wamekuwa wakihangaika kufuata huduma za upasuaji wilayani songea.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Dkt Yuna Hamis amesema kuwa msaada wa mifuko hiyo ya saruji utasaidia kukamilisha jengo la upasuaji na wodi ya wazazi na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Bw. Christpher Kirungu ameshukuru kwa msaada huo.