Back to top

Kiongozi wa mbio za mwenge agoma kukabidhi hundi ya mikopo kwa vijana

08 May 2018
Share

Utoaji wa mkopo wa shilingi Milioni mbili kwa vikundi vya vijana, wa kata za Nkandasi na Chala wilayani Nkasi mkoani Rukwa umeingia dosari, baada ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Charles kabeho, Kugoma kutoa rasmi hundi hiyo kufuatia baadhi ya vijana kushindwa kuthibitisha umri wa miaka 35, unaotambulika kisheria kwa vijana nchini.
 
Sakata lilianza baada ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa Bw Charles Kabeho, kuombwa kutekeleza utoaji rasmi wa mkopo na ndipo alipowataka vijana hao kuthibitisha kama wanakidhi vigezo,na ndipo idadi kubwa waliposhindwa kufanya hivyo, naye kutoa maamuzi yasiyo ya kawaida kwa kuwapa muda.
 
Hata baadaye aliporejea baada ya kukagua miradi mingine miwili,akakutana na vijana sita wenye barua za utambulisho kutoka kanisani kinyume cha sheria,na ndipo alipofikia kutoa maamuzi magumu.