Back to top

DC Handeni azindua chanjo ya saratani.

08 May 2018
Share

Wazazi na walezi wa watoto wa wilaya za Handeni na Korogwe mkoani Tanga wametakiwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya saratani huku serikali ikiahidi kuhakikisha watoto wote ndani ya wilaya hizo wanapatatiwa chanzo hiyo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe ambae pia ndie kaimu mkuu wa wilaya ya Korogwe wakati akizindua zoezi hilo la kuwa patia chanjo hiyo ya saratani kwa wanafunzi hao uzinduzi huo umefanyika shule ya sekondari Old Korogwe iliopo wilayani Korogwe na kuhudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali pamoja na wazazi. 

Hata hivyo mkuu huyo akaonya kuwa chanjo hiyo ni bure na asitokee mtu akawa anachangisha fedha kwaajili ya huduma hiyo. 

Nae Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Korogwe amesema wanatarajia kuchanja zaidi ya wanafuzi mia saba huku baadhi ya wazazi wakiipongeza serikali na kuomba hamasa iongezwe ili kuondoa imani potofu walizo kuwa nazo baadhi ya wazazi.