Serikali imesema imefuta tozo saba kwenye mbegu bora katika kipindi cha mwaka 2017/18 ili kupunguza gharama za uzalishaji,kuongeza upatikanajai wa kupunguza bei ya mbegu bora kwa mkulima.
Akijibu swali la Mbunge wa Mpanda mjini,Mheshimiwa Sebastin Kapufi aliyeuliza ni lini serikali itahakikisha inasambaza pembejeo kwa wakati na kuzingatia msimu na jiografia ya maeneo husika.
Naibu Waziri wa kilimo Mheshimiwa Mary Mwanjelwa amesema kufuta kwa tozo hizo serikali inategemea bei ya mbegu bora itapungua na wakulima wengi wataweza kununua na kutumia.
Amesema serikali imeendelea kuandaa mifumo ya kuhakikisha kwamba pembejeo za kilimo zinasambwaza na kuwafikia wakulima kwa wengi kwa wakati na kwa bei nafuu,ambapo ili kufikia malengo hayo pia serikali imeanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja ili kuhakikisha mbolea inapatikana na kusambazwa kwa wakulima kwa wakati.
Aidha amesema serikali kesho inatarajia kutoa semina kwa wabunge kuhusu mfumo wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja-BPS- ili kuwajengea ufahamu kwa wote.