
Serikali imesema itaendelea kutoa fedha za kifuta jasho kwa uharibifu wa mali na kifuta machozi kwa wahanga waliouawa au kujeruhiwa na tembo katika jimbo la Mtera.
Akijibu swali la Mbunge wa Mtera Mheshimiwa Livingstone Lusinde aliyeuliza ni serikali inampango gani juu ya wanyamapori waharibifu hususani tembo ambao wamesambaa ovyo katika jimbo la Mtera na kufanya uharibu mkubwa pamoja na kuua watu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga,katika mwaka 2017/18 Wizara ya Maliasili na Utalii imelipa jumla ya shilingi milioni 7.5 kwa wananchi 27 wa wilaya ya Chamwino walioathirika na wanyamapori.
Amesema ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu mali na vifo serikali itaendelea kufanya doria za kudhibiti wanyamapori katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chamwino, pamoja na kutoa elimu ya njia nyingine za kudhibiti tembo zikiwemo matumiziya mzinga ya nyuki,uzio wa kamba iliyopakwa mafuta machafu na pilipili.
Aidha Mheshimiwa Hasunga amesema ongezeko la watu limesababisha kuzibwa kwa shoroba za wanyamapori pamoja na maeneo ya mazalia na matawanyiko yao,ambapo kuzibwa na shorona hizo kumesababisha kuongezeka migongano baina ya binadamu na wanyapori.