Serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.Wiliam Lukuvi imetangaza mpango wake wa kuwamilikisha ardhi ikiwa ni pamoja na kuwapatia hati za umiliki wananchi wanaoishi katika eneo la boko kwa somji jijini Dar es Salaam lenye ukubwa wa ekari 366.
Taarifa ya Waziri wa Ardhi inasema hati ya kwanza ya eneo hilo ilitolewa na serikali mwaka 1952, ambapo umiliki wa Somji ulitambulika mwaka 1971 kabla ya serikali kutangaza kulitwaa eneo hilo la ekari 366 mwaka 2002 kwa manufaa ya umma ambapo kwa muda wote huo wananchi wamekuwa wakiishi kwa hofu kama wavamizi wa eneo la seriklai.
Akiwa katika eneo hilo la Boko Waziri Lukuvi ametangaza rasmi eneo hilo kupimwa, kupangwa na baadae wananchi kumilishwa kwa kupatiwa hati za umiliki na kusema sasa fedha za fidia ambazo seriklai ilipaswa kumlipa Somji zitalipwa na wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi ametangaza marufuku ya uuzwaji ama uendelezaji wa maeneo ndani ya eneo hilo la ekari 366 huku mbunge wa kawe akiwataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa maafisa ardhi wa seriklai na kamati iliyoundwa na wananchi.
Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi zoezi hilo la upimaji,upangaji na urasimishwaji yanapaswa kukamilika mapema mwezi septemba mwaka huu chini ya uratibu wa maafisa ardhi wa serikali na kamati iliyoundwa na wananchi wa eneo hilo.