Back to top

Viwavi vyateketeza zaidi ya hekta Elfu ishirini za mahindi Mvomero.

18 May 2018
Share

Zaidi ya hekta Elfu ishirini sawa na ekari elfu hamsini za  mashamba ya mahindi ya wakulima wadogo katika vijiji vya wilaya ya Mvomero  zimeteketezwa  kwa kuliwa na wadudu waharibifu wa mimea  aina ya Viwavi Jeshi vamizi Fall Armyworm.

Baadhi ya wakulima ambao mashamba yao yamevamiwa na Viwavi Jeshi vamizi wanasema wamepata hasara kubwa katika msimu huu wa kilimo hali iliyowakatisha tamaa ya kuendelea na shughuli ya kilimo .

Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wilaya ya Mvomero Daina Mnywanga anasema tatizo ni kubwa.

Baada ya kutembelea eneo lililoathirika  na kutoa elimu kwa waafisa ugani wakulima pamoja na wakala wa pembejeo za kilimo mtafiti wa wadudu waharibifu na viutilifu kutoka TPRI anasema hadi sasa zaidi ya mikoa kumi na sita imesha athirika na wadudu hao  na kwamba tpri imeshapata viuatilifu vyenye uwezo wa kuua wadudu hao na wanaendelea kutoka elimu.