Idara ya Magereza katika mkoa wa Kagera leo imemuaga rasmi Naibu Kamishina Mhandisi Jeremia Nkondo ambaye pia alikuwa mkuu wa Magereza katika mkoa huo pamoja na maofisa wengine 60 wa idara hiyo akiwemo kamishina msaidizi Zakharia Kumalija ambao wanastaafu baada ya kumaliza muda wao wa utumishi.
Naibu Kamishina Mhandisi Nkondo na Maofisa wengine ameagwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa mashujaa ulioko katika manispaa ya Bukoba na kupambwa na gwaride maalumu lililoandaliwa na maofisa wa idara hiyo na maonyesho ya utayari yaliyofanywa na kikosi maalumu cha kupambana na vurugu ndani ya Magereza ambayo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa magereza wa mikoa ya kanda ya ziwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhadisi Nkondo amewahimiza maofisa wa jeshi hilo kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa huku, Kumalija akiwashauri maofisa magereza wanaoendelea na utumishi kuzingatia nidhamu.
Kwa upande wao, baadhi ya wakuu wa Magereza kutoka mikoa ya kanda ya ziwa walioudhuria hafla hiyo ambao wamezungumza wamemulezea Mhandisi Nkondo kuwa alikuwa mchapa kazi na mtu aliyekuwa akiheshimu kazi yake na kuwajali maofisa wenzake.