Back to top

Mkuu wa mkoa wa Tanga apiga marufuku Stand bubu Korogwe.

02 June 2018
Share

Baada ya kituo cha ITV kuripoti uwepo wa Stand bubu ndani ya halmashauri ya mji wa Korogwe hali iliokuwa ikidhoofisha mapato ya halmashauri hiyo hatimaye mkuu wa mkoa wa Tanga amepiga marufuku uwepo wa Stand hizo.

Mkuu huyo ameyasema hayo baada ya kusikiliza pande zote tatu wakiwemo wataalam wa halmashauri madiwani pamoja na viongozi wa chama cha wasafirishaji waliopo Stand mpya ambayo ilizinduliwa mwezi wa nane mwaka jana na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jonh Pombe Magufuli amesema kuwa kuanzia sasa Stand iwe ni moja na hali hiyo itaiongezea mapato halmashauri hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa akatoa maagizo ya kutatua baadhi ya changamoto ambazo zilikua kero kwa baadhi ya wasafiri pamoja wasindikizaji kwenye Stand hiyo mpya amemwagiza Mkurugenzi kuondoa ushuru wa shilindi miambili na kuahidi kutoa bati mia moja kwaajili ya kujenga mabanda ya mama lishe kwenye Stand hiyo.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jumanne shauri alimwelezea mkuu huyo namna halmashauri hiyo ilivyokuwa ikipoteza mapato kupitia Stand bubu.

Mvutano huo wa Stand ambao ulikuwa ukipelekea mgawanyiko mkubwa ndani ya halmashauri hiyo ambapo ilionekana kuwa baadhi ya madiwani wakiungana na Mwenyekiti wao walikuwa wakipendelea Stand ya zamani iendelee kupokea magari hali ambayo ilikuwa ikidhoofisha Stand mpya.