Back to top

Afisa Mkuu wa biashara wa Tigo afanya ziara IPP Media

19 September 2019
Share

Afisa Mkuu wa biashara wa Tigo Bw.Tarik Boudiaf amefanya ziara katika vyombo vya habari vya IPP(The Guardian,ITV/Radio One,East Africa Tv/Radio na Capital Radio) ili kuona namna ya habari na vipindi mbalimbali vinavyotayarishwa.

Akizungumza baada ya ya ziara hiyo Bw.Boudiaf amesema kuwa amefurahishwa kuona kampuni hii imewekeza kwa kiwango kikubwa katika teknolojia ya habari jambo ambalo linakwenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia

Ziara hiyo imekuwa ni sehemu ya mahusiano mazuri kati ya kampuni ya Tigo na IPP Media huku Bw.Boudiaf akisisitiza kuendeleza uhusiano huo kibiashara.