Back to top

Hatma ya makubaliano mapya ya BREXIT kujulikana Oktoba 19.

18 October 2019
Share

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anapanga kutoa taarifa kuhusu makubaliano mapya ya mpango wa nchi yake kujitoa umoja wa ulaya kwenye bunge la Uingereza siku ya Jumamosi. 

Kwa mujibu wa kiongozi wa wabunge Jacob Rees- Mogg wabunge watajadili iwapo wapitishe mpango mpya wa BREXIT ama nchi hiyo kujitoa kwenye umoja huo bila makubaliano. 

Naye kiongozi wa mazungumzo hayo upande wa Umoja wa Ulaya Michel Barnier, ameyapongeza makubaliano hayo akisema yanalinda maslahi ya Ulaya lakini pia ametahadharisha kuwa makubaliano hayo yanapaswa kupitishwa na bunge la Uingereza ambalo limeshayakataa makubaliano ya Brexit mara tatu.