
Serkali mkoani Geita imeanza kugawa vitambulisho zaidi ya elfu sitini kwa wafanyabishara wadogo kwa wilaya tano za mkoa huo huku ikitumia mfumo wa kielektroniki katika kuwasajili wafanyabiashara ili kudhibiti vitendo vya kudurufu pamoja na kuazimana vitambulisho ili kudhibiti vitendo vya uchakachuaji.
Akikabidhi vitambulisho hivyo kwa wakuu wa wilaya za mkoa huo mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabrieli anasema serikali kwa kushirikia na TRA wamelazimika kutumia mfumo huo ili kudhibiti vitendo vya uchakachuaji.
Kaimu meneja wa TRA mkoa wa Geita Mtware Mazura anasema awamu ya kwanza wameanza na zoezi la kuwapatia vitambulisho elfu kumi na mbili huku awamu ya pili ikianza mwishoni mwa mwezi huu ili kuhakikisha kila mfanya biashara anafikiwa.
Wakizungumza mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo vya wajasiriamali wakuu wa wilaya wamewataka wafanyabiasha ambao wameanzisha biashara mpya wajitokeze kusajiliwa ili kuondoa usumbufu kutoka kwa TRA.