Back to top

CCM kuwabana watoa rushwa mchakato kuwapata wagombea wa chama hicho

05 August 2020
Share

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama juu ya uwepo wa vitendo vya rushwa katika mchakato wa kuwapata wagombea wa chama hicho katika ngazi mbalimbali na kwamba chama kitamchukulia hatua yeyote atakayethibitika kuhusika na ukiukwaji wa kanuni na katiba ya CCM.

Bw.Polepole pia amesema kwa sasa chama hicho kinaendelea na michakato kulingana na ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi huku mgombea wa Urais wa CCM Rais Magufuli akitarajiwa kuchukua fomu katika ofisi za NEC ndani ya wiki hii.