
Joe Biden ashinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump.
Bw. Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania kwa kupata kura zaidi ya 270 zilizohitajika.
Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa Rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.