Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa Rais.
.
Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20.
.
Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.
.
Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.
BBC Swahili