Back to top

Rais Mwinyi asisitiza kuongeza makusanyo ya kodi.

12 January 2021
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta Hussein Ali Mwinyi  amesisitiza dhamira ya serikali anayoingoza ya kufungua uchumi na kuongeza makusanyo ya kodi, ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi.
.
Amesisitiza hayo alipolihutubia taifa kutoka viwanja vya  Mnazi Mmoja mjini Zanzibar katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
.
Amesema katika kufungua uchumi, serikali inakusudia kuwavutia wawekezaji, kupanua uwekezaji na  kuimarisha uvuvi wa kisasa kwa kutumia kikamilifu rasilimali kuu ya bahari ambayo Zanzibar imejaliwa kuwa nayo.
.
Aidha, ameelezea azma ya serikali ya kuimarisha ukusanyaji wa kodi ambayo pamoja na mambo mengine itasaidia kupanua huduma za elimu na afya na kuongeza kiwango cha malipo kwa wazee.
.
Rais Dakta Mwinyi amerudia wito wake kwa wananchi wa kutimiza wajibu wao na kutoa  ushirikiano kwa serikali ya umoja wa kitaifa aliyoiunda kwa mujibu wa katiba, ili kuiwezesha kuwaletea maendeleo na ustawi wa wananchi.