Back to top

RONALDO ATUPIA HAT TRICK YA 57

15 March 2021
Share

Licha ya habari kuenea kuwa Juventus wanampango wa kumuuza mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo hatimaye mshambuliaji huyo amefunga Hat Trick ya 57 katika maisha yake ya soka wakati Juventus wakishinda bao 3-1 dhidi ya Cagliari katika Serie A hapo jana.

Ronaldo amefunga Hat Trick hiyo ndani ya dakika 32 pekee na kuirejesha Juventus katika ubora wake kwa ushindi wa ugenini baada ya kutolewa katika michuano ya Ulaya wiki iliyopita.

Awali kabla ya mchezo huo Ronaldo aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa "Bingwa wa kweli hapumziki" na kusisitiza kuwa wamesahau yaliyopita na sasa wanaangalia namna ya kutwaa makombe mengine kama vile ligi ya Italy Serie A na kombe la Italia na mengineyo msimu huu.

Juventus sasa wanashika nafasi ya 3 wakiwa na alama 55 nyuma ya vinara Inter Milan wenye alama 65.