Back to top

Wazee Babati walalamikia milio ya pikipiki. 

05 April 2021
Share

Baadhi ya wananchi wakiwemo wazee wenye matatizo ya kiafya katika Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wamelalamikia tabia ya baadhi ya waendesha bodaboda waliobadilisha milio halisi ya pikipiki na kuweka inayofanana na milio ya milipuko na kuliomba Jeshi la Polisi kukomesha vitendo hivyo.
 
Wakizungumzia changamoto hiyo inayowaathiri kiafya licha ya kuwataka baadhi ya wanasiasa kuacha kuingilia zoezi hilo lenye baraka ya Mkuu wa mkoa Joseph Mkirikiti kupitia kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa. 

Naye Mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda mkoa Manyara Bw Omari Bakari amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo ambavyo pia vinawafanya baadhi ya madereva kuondoa vipuri na kukiuka sheria za usalama barabarani.