
Wazara ya Mali Asili na Utaliii imetenga shilingi bilioni 75 kwa ajili ya kukarabati miundombinu yote chakavu ikiwemo barabara katika hifadhi na vivutio vyote vya utaliii vilivyopo katika mikoa kusini mwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021//2022.
Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe.Mary Francis Masanja ameyasema hayo wakati akijibu swali la Dokta Ritta Kabati Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa aliyetaka kujua serikali ina mpango gani kuendeleza maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania utaanza.
Mhe.Masanja amesema mpango huo inakwenda sawia na kutenga shilingi bilioni 46.5 kwa ajili ya kutangaza vivutio vyote vya mikoa ya kusini kwa ajili ya kuhakikisha maliasili hizo zinaleta tija na kuchangia kuongeza pato la taifa kupitia vivutio hivyo.
Kadhalika Naibu Waziri huyo wa Mali Asili na Utalii amewaonya wafugaji kuacha mara moja vitendo vya kuchungia mifugo yao ndani ya hifadhi mbalimbali kwa kuwa kitendo hicho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria za uhifadhi wa mali asili.