Mgomo wa madereva wa kiwanda cha saruji cha Dangote zaidi ya mianne umefikia siku ya kumi sasa, huku serikali ya mkoa ikigonga mwamba licha ya kufanya vikao vitatu ili kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili ikiwemo maslahi bora ya kazi na hivyo kuomba viongozi wa kitaifa kuingilia kati huku hitaji lao kubwa likiwa ni kuwaondoa mawakala wa usafirishaji ili kiwanda kiajiri madereva moja kwa moja.
.
Kauli hiyo wameitoa mara baada ya kumaliza kikao na mkuu wa mkoa na kusisitiza kuendeleza mgomo licha ya baadhi ya changamoto kupatiwa ufumbuzi.