Back to top

Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro wapewa siku 7 kurekebisha mikataba.

18 April 2021
Share

Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa siku saba kwa uongozi wa Mkoa wa Killimanjaro kuhakikisha unarekebisha kasoro zilizo kwenye mikataba ya shamba la kutunzia wanyamapori yatima la Makoa, kabla ya kupewa kibali cha kuleta Simba kutoka nje ya nchi kwa ajili ya matunzo.

Akizungunza baada ya kutembelea shamba la Wanyamapori la Makoa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema shamba hilo linapokea wanyamapori yatima na majeruhi kutoka kwenye hifadhi zote hapa nchini.

Amesema kutokana na umuhimu wa shamba hilo, ipo haja ya Serikali ya Mkoa kusaidia Chama cha Ushirika cha Urudu Makoa ili kifahamu  namna sahihi ya kuingia mikataba yenye tija kwa taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira amesema kumekuwa na ukakasi wa kufahamu Mwekezaji halisi ni nani ili kuingia mkataba jambo ambalo baada ya Waziri kufika kila kitu kimekuwa wazi.