
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imepokea na kuridhia kusikiliza maombi ya Bw.James Mbatia ya kupinga utaratibu wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai kwamba hakufuata misingi na taratibu ambazo zimeelekezwa na katiba zinazotakiwa kufuatwa pale Spika wa Bunge atataka kujiuzulu wadhifa wake.
