
#HABARI: Kufuatia tukio la watu watano wa familia moja kuuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma, Mkuu wa Mkoa huo Bw. Anthony Mtaka amefika eneo la tukio ambapo ameviagiza vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina huku akiwataka wananchi hao kujitafakari kutokana na tukio hilo.
