
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi amewataka Waratibu wa chanjo wa mikoa kuongeza vituo vya kutolea huduma za chanjo katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za chanjo.
.
Prof. Makubi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa tathmini ya chanjo ngazi ya Mkoa unaofanyika Manispaa ya Morogoro.
