Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi wenye ushahidi mwingine wa ziada na wenye kuthibitisha kuwa kuna uhalifu mwingine uliofanywa na askari saba wanaotuhumiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamis mkoani Mtwara kufika katika timu inayofanya uchunguzi huo ili ushahidi huo uweze kuchukuliwa.

