
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge na Uratibu, Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyopo Ndejengwa jijini Dodoma Januari 27, 2022 akiwa na lengo la kuona namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavyofanya kazi na kutekeleza majukumu yake.

Waziri Balozi Dkt.Chana alipokelewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Charles Mahera ambaye alimtembeza maeneo mbalimbali ya ofisi hizo na baadaye kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Katika Ziara hiyo Waziri Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga na Viongozi wengine waandamizi wa wizara hiyo.
