Back to top

TANESCO yatangaza mgao wa umeme kwa siku kumi.

28 January 2022
Share

Shirika la Umeme Nchini(TANESCO) limetangaza mgao wa umeme wa siku 10 kuanzia Februari 01, 2022 kutokana na marekebisho katika bomba la gesi kutoka Songosongo na TPDC huku Shirika hilo likibainisha kuwa hali ya uzalishaji wa umeme imeimarika kiasi ikilinganishwa na mwezi uliopita ambapo uzalishaji ulishuka kufuatia mvua kukosekana.