
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewaagiza watendaji wa Kata, madiwani na wenyeviti wa vijiji kufanya oparesheni ya nyumba kwa nyumba kuwasaka wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti katika shule walizopangiwa baada kutoridhishwa na idadi ya wanafunzi walioripoti tangu shule zifunguliwe Januari 17, 2022.
