
Wakili wa upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Peter Kibatala ameendelea kumhoji shahidi wa 12 wa upande wa mashtaka Luteni Urio ikiwa ni siku ya tatu mfululizo ambapo amemuhoji kuanzia asubuhi hadi jioni na hivyo Jaji Joachim Tiganga kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 01, 2022.
.
Hata hivyo kabla ya Jaji Tiganga kuahirisha kesi hiyo, Wakili Kibatala alitoa hoja ya kuomba kesi iahirishwe mpaka kesho akidai kuwa bado ana maswali mengi.
