
Rais Umaro Sissoco wa Guinea- Bissau amesema jaribio la kuiondoa serikali yake madarakani halikufanikiwa kwa sababu anaungwa mkono na wananchi walio wengi.
Amesema jaribio hilo lilifanyika wakati Baraza la Mawaziri likiwa katika kikao cha dharura na Rais na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nuno Gomes Nabiam.
Rais Umaro Sissoco amesema jaribio la mapinduzi lililokusudiwa kumuondoa madarakani limeshindwa, hivyo amewataka wananchi kote nchini humo wawe watulivu.
Amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku serikali yake ingekumbwa na hali kama hiyo na hakuwahi kudhani kwamba wananchi wa nchi hiyo wanaweza kutekeleza kitendo kingine cha kuibua machafuko.
