Back to top

IGP Sirro amuagiza Awadhi kumaliza uhalifu Zanzibar.

02 February 2022
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemuagiza Kamishna wa Polisi Zanzibar Awadhi Juma Haji kuhakikisha anakwenda kumaliza changamoto za makosa ya dawa za kulevya, makosa ya udhalilishaji pamoja na makosa mengine ya uhalifu yanayojitokeza Zanzibar.


IGP Sirro ameyasema hayo wakati akimvalisha cheo na kumuapisha Kamishna huyo ambaye alipandishwa cheo na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.