Back to top

Kesi ya Mbowe: Kibatala aweka rekodi

02 February 2022
Share

Kiongozi wa jopo la Mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Wakili Peter Kibatala ameweka rekodi ya kutumia muda mwingi zaidi kumhoji maswali shahidi wa 12 upande wa mashtaka Luteni Denis Urio kuliko shahidi mwingine yeyote katika kesi hiyo ambapo ametumia jumla ya saa 11 na dakika mbili kumuhoji shahidi huyo.

Wakili Kibatala na waendesha mashtaka wametumia muda mrefu kwa shahidi huyo ambaye ni Afisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi maalumu (makomando) kilichopo Ngerengere, mkoani Morogoro, kwa sababu yeye ndiye msingi wa kuwepo kwa kesi hiyo.